Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe leo July 10, 2017 ametangaza kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Dionis Malinzi.
Maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupitia upya utekelezaji wa Baraza hilo katika michezo nchini, hivyo Waziri Mwakyembe amesitisha uteuzi huo ili kujiridhisha kuhusu utendaji wa Baraza hilo.
Kama utakumbuka vizuri July 5, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha Bunge hadi September 5, 2017 ambapo alimuagiza Waziri Mwakyembe kufanya mapitio ya uteuzi wa Baraza hilo.
Waziri Mwakyembe amesitisha uteuzi wa mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Dionis Malinzi #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/KtYansPQ27
— millard ayo (@millardayo) July 10, 2017
VIDEO: Taifa Stars ilivyopokelewa, Kocha Mayanga kathibitisha wamemuacha mchezaji South