Mbunge wa Kawe, Halima Mdee baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku tano leo July 10, 2017 alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka moja la kumkashifu Rais.
Halima Mdee alisomewa kosa hilo na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ambapo alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo July 3, 2017 akiwa Makao Makuu ya CHADEMA DSM.
Baada ya kuahirishwa kesi hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kuizungumzia issue hiyo.
>>>”Mdee amesomewa mashtaka ambayo sitaki kuyazungumzia, lakini utamaduni huu mpya unaojengwa ndani ya taifa wa kuziba midomo watu wasiseme hisia zao, utajenga chuki katika jamii. Sisi kama chama cha kupigania haki tunaamini, kila MTU ana haki ya kueleza hisia zake.
“Halima ni mbunge pia ni kiongozi mwandamizi, wakati alivyozungumzia suala la wanafunzi kupata mimba alikuwa akizungumzia kama mwanamke. Hivyo, kama chama kitaendelea kuzungumza bila kujali Polisi na Wakuu wa Wilaya wanatumia sheria ipi. Kama chama kitaendelea kuzungumza bila woga, kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli. Tunaamini huku ni kuipotezea muda Serikali pamoja na Mahakama. Time will tell.” – Freeman Mbowe
GUMZO LA ESCROW: Sababu 5 za William Ngeleja kurudisha Fedha za ESCROW!!