Hivi karibuni Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ imekuwa inawekeza nguvu kwenye ukusanyaji wa mapato ambayo imekuwa inahakikisha kila mwananchi analipa kodi hasa kwa kutumia risiti za kielektroniki ‘EFD’.
Leo July 11, 2017 Mamlaka hiyo imetoa ripoti yake ya makusanyo ya kodi kwa mwaka 2016/2017 ambapo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi Richard Kayombo amesema Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 14.4 kwa mwaka wa fedha 2016/17 ambapo kuna ukuwaji wa 7.67% huku makusanyo ya mwezi June 2017 pekee yakiwa ni Tsh. Tirioni 1.37.
Aidha, Richard Kayombo amesema kwamba TRA imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo huku ikiwashukuru Watanzania kwa mwitikio mkubwa na waendelee kujitokeza kwenye Ofisi mbalimbali za TRA nchi nzima ili waendelee kulipa kodi.
>>>“Mamlaka inapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za EFD pindi wanapouza bidhaa au huduma na wanachi wote wahakikishe wanadai risiti pindi wanaponunua bidhaa au huduma. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.” – Richard Kayombo
Kama ulimdhamini mtu Mkopo Elimu ya Juu hii inakuhusu (+Video)