Jumanne ya July 11 2017 kocha wa zamani wa wekundu wa Msimbazi Simba muingereza Dylan Kerr amewasili Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya kufukuzwa na Simba Janury 12 2016 kufuatia kutolewa katika michuano ya Mapinduzi Zanzibar.
Dylan Kerr amewasili Dar es Salaam safari hii akiwa na timu ya Gor Mahia kama kocha mkuu wa timu hiyo na amekuja Tanzania kuongoza kikosi chake cha Gor Mahia kucheza game ya kirafiki dhidi ya Everton katika mchezo utakaochezwa July 13, Kerr ameizungumzia Tanzania na Simba.
“Naipenda hii nchi na imekuwa furaha sana kwangu kurudi tena kwa sababu sikuwahi kupata nafasi ya kuwaaga watu tofauti tofauti wakati naondoka hususani mashabiki wa Simba licha ya kuwa nimejiunga na Gor Mahia nimekuwa nikipokea meseji zao kupitia twitter account yangu kitu ambacho kinanipa furaha sana”>>> Kerr
“Kucheza na Everton ni fursa kubwa sana na ni nafasi kwa wachezaji kuonesha vipaji vya Afrika Mashariki kwa Everton lakini kwa dunia nzima pia ambapo watu watakuwa wanaangalia”>>> Kerr
EXCLUSIVE: Staa wa Bundesliga mwenye asili ya Tanzania kwanini anachezea Denmark na sio Tanzania