Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kujitosa kwenye mgogoro wa Chama cha Wananchi CUF, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya ameibuka na kusema hawatazivumilia hujuma za chama hicho.
Akizungumza katika Ofisi za CUF Makao Makuu Buguruni, Sakaya amesema mara kadhaa wameripoti matamko ya viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiingilia mgogoro wa CUF.
“Chadema wamekuwa na vikao kadhaa na mkakati wa kuhakikisha wanaifuta CUF upande wa Bara, miongoni kwa mipango hiyo ni kuvamia Ofisi pamoja na kuratibu na kukusanya vijana wa kihuni.” – Magdalena Sakaya.
Aidha, Sakaya amesema kuwa CUF wanalichukilia jambo hilo kuwa ni kushindwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi kuiuza CUF kwa Chadema.
“Tunawataka Watanzanua wafahamu kuwa CUF ni chama kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria na kina Katiba yake. Hivyo hatutotoa fursa ya kufanyiwa maamuzi nje ya vikao vya chama na tunatoa onyo kwa viongozi wa CHADEMA.” – Mgdalena Sakaya.
EXCLUSIVE: Majibu ya Tundu Lissu kuhusu kumfuta uanachana Waziri Mwakyembe!!!