Brigedia Jenerali mstaafu Dominic Mrope amewataka Wanajeshi kuwa na nidhamu, utii, uhodari pamoja na uzalendo kwa kuwa kazi hiyo inatakiwa kufanywa kwa ajili ya uzalendo.
Brigedia Jenerali Mrope alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya JWTZ ambapo amesema uzalendo ni kitu kikubwa ambacho ni kama dini ya Jeshi hasa kujitoa maisha katika kipindi chote cha uhai kwa kuwa hata yeye alijitoa katika kipindi cha takribani miaka 38.
“Nawaasa wadumishe utii na uzalendo…mafunzo ya kijeshi yahanitaji ukakamavu, afya na utimamu kwani bila hivyo huwezi kufanya mafunzo yoyote.” – Brigedia Jenerali mstaafu Dominic Mrope.
Tamko la CUF kuhusu hujuma zinazofanywa na CHADEMA!!!