July 13, 2017 stori nyingi zimeripotiwa kwenye Televisheni, Radio, Magazeti na Mitadao mbalimbali ambapo miongoni mwa stori hizo ni issue ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kurudi tena Polisi leo huku viongozi wa CHADEMA wakiahidi kumsindikiza.
Nimekukusanyia na kukusogezea karibu stori zote kubwa asubuhi ya leo kupitia millardayo.com.
Mkazi wa kijiji cha Kizingwangoma, Sengerema Benadeta Kulwa amejinyonga kwa kanga baada ya kumjeruhi mumewe kwa wivu wa mapenzi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Bodi ya Wadhamini wa NSSF imetangaza kuwaachisha kazi vigogo 12 wa shirika hilo waliosimamishwa kazi July 2016 kupisha uchunguzi. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango ameiagiza TRA kufanya ukaguzi nchi nzima kubaini wamiliki wa vituo vya mafuta wasiofunga EFD. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga, Rukwa wakituhumiwa kuwateka watoto wadogo na kuwapa mafunzo. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Polisi Shinyanga inafanya uchunguzi kuwabaini watu waliochoma moto pikipiki ya Serikali mali ya Halmashauri ya Ushetu, Kahama. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Mohammed Mpinga ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Imeelezwa kuwa njia pekee ya Serikali kufanikisha uchumi wa viwanda ni kuwawezesha vijana wanaohitimu elimu katika vyuo mbalimbali. #MAJIRA
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Wakazi wa maeneo mbalimbali ya DSM jana walijitokeza kuuaga mwili wa Mtangazaji wa EFM Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma. #MAJIRA
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Serikali itabadili matumizi ya ofisi za Mifugo ya Halmashauri ya Mbulu, Manyara kwa kufungua kituo cha Polisi katika pori Tengefu. #MAJIRA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Mwili wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kereba, Tarime, Marwa Wankuru umekutwa kwenye bwawa la maji ukiwa umefungwa mikono na jiwe. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Serikali imetoa vibali vya ajira 10,184 kujaza nafasi za waliobainika kughushi vyeti miezi miwili baada ya ripoti ya uhakiki. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Watumishi wa Serikali wasiopeleka vyeti vyao kuhakikiwa hawatolipwa mishahara mpaka watakapopeleka vyeti hivyo ili kuhakikiwa. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Taasisi ya Tulia Trust imesema itajenga mabweni ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari ya Masoko, Wilayani Rungwe, Mbeya. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Taasisi ya Albino Enterprises of Dar es Salaam imemuomba Rais JPM kuwapatia mkopo wa Tsh. 100 milioni iweze kufungua viwanda vidogo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Serikali imetengea Tsh. trilioni 1 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati ya umeme. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
CHADEMA imeendelea kupata pigo baada ya viongozi wake 84 ktk Wilaya ya Misungwi, Mwanza kufunga Ofisi za chama hicho na kuhamia CCM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
CUF imetangaza vita dhidi ya CHADEMA baada ya kudai kufanyiwa hujuma na kuchochea kufanyika vurugu na kuingilia mgogoro wao wa ndani. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wadogo kuwa itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Watu wawili wameuawa na miili yao kuchomwa moto ktk kijiji cha Mao, Kalambo, Rukwa wakituhumiwa kwa wizi wa ng'ombe 16. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Mawakili wawili wa Serikali hawakufika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwenye kesi ya rufaa iliyofungulliwa na Mbunge Lema. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Viongozi wa CHADEMA leo watamsindikiza aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye ataripoti Makao Makuu ya Polisi DSM. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Watanzania wametakiwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rasi Magufuli ili lengo la kuwatumikia litimie. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Serikali imewanasa walimu wapya 2,700 wenye vyeti feki baada ya uhakiki wa pili ktk ajira mpya zilizotangazwa April mwaka huu #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
BAADA ya hivi karibuni CHADEMA kutangaza kuingilia kati mgogoro unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi CUF ili kuhakikisha wanamuondoa madarakani Mwenyekiti anayetambulika na Msajili, Prof. Lipumba, CUF nayo imetoa Tamko kuhusu hujuma inazodai zinafanywa na CHADEMA…bonyeza PLAY kwenye hii VIDEO kutaama!!!