Leo July 13, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya kutakatisha fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba SC Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi July 20, 2017 kutokana na upelelezi kutokamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa baada ya Wakili wa Serikali Christophe Msigwa kusema upelelezi haujakamilika hivyo wanaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi July 20, 2017 ambapo aliutaka upande wa Serikali kukamilisha upelelezi.
Kesi ya kutakatisha fedha na inayomkabili Rais wa Simba, Aveva na makamu wake, Kaburu imeahirishwa hadi July 20, upelelezi haujakamilika. pic.twitter.com/5LMsbljMlO
— millardayo (@millardayo) July 13, 2017
Wayne Rooney na kikosi cha Everton walivyowasili Tanzania!!!