Mapema leo kulikuwa na stori kuwa TRA Mwanza imeifungia Kampuni ya Sahara Media inayomiliki Star TV, RFA na Kiss FM wakiidai malimbikizo ya kodi ya zaidi ya Tsh. Bilion 4 wakiitaka kulipa ndani ya siku 14 vinginevyo kampuni itapigwa mnada.
Baada ya taarifa hizo Meneja Rasilimaliwatu wa Sahara, Rafaeli Shilatu amekiri kufungiwa akidai ni kutokana na malimbikizo ya kodi baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya wakati wa kuhama kutoka analogy kwenda Digital ingawa wanajitaidi kuhakikisha kwamba wanarudi hewani na kulipa kodi kama kawaida.
>>>”Lazima tukiri kwamba mmeshuhudia TRA wamefunga maeneo yetu ya kazi na hii inatokana na malimbikizo ya kodi ambayo siyo ya sasa ni ya muda mrefu hata nyie waandishi wa habari mnajua kwamba kadri uwekezaji unavyokuwa mkubwa ndivyo gharama zinazidi kwenye uwekezaji. So, ilitulazimu kutafuta fedha kwenye mabenki ili tuweze kukidhi matakwa ya Serikali ya kuhama analogy kwenda Digatal.
“Niwatoe wasiwasi Watanzania na wapenzi wa Sahara hili ni jambo la muda lakini kampuni yetu inafanya jitihada kuhakikisha kwamba haya yanamalizika vyombo vyetu virudi hewani.” – Rafaeli Shilatu
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story
VIDEO:Lowassa alivyotumia dakika 30 kuingia na kutoka Makao Makuu ya Polisi