Tayari nimekukusanyia uchambuzi wa stori zote kubwa za magazeti ya Tanzania leo July 15, 2017 ambapo kila siku huwa nazipandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Hatma ya kesi mbalimbali za Chama cha Wananchi CUF itajulikana August 11 wakati Mahakama Kuu Kanda ya DSM itakapotoa uamuzi. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
RC Anna Mghwira amewaonya Wakurugenzi wa Halmashauri 6 za Kilimanjaro kuacha tabia za kizamani kutowapa taarifa madiwani wao. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Serikali haitowahurumia viongozi na watendaji wa vyama mbalimbali vya msingi, ushirika wenye tabia ya kuwaibia wakulima fedha zao. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Watu wawili katika Tarafa ya Kasamwa, Geita wamefariki baada ya kukosa hewa wakiwa ndani ya shimo walilokuwa wanachimba kisima. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Mahakama ya Tanzania imeagizwa kuhakikisha inamaliza vitendo vya rushwa bila woga kwa kuwa wanachangia kupoteza imani kwa wananchi. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
CHADEMA imesema mkakati wa kuviua vyama vya upinzani unaofanywa na CCM utakwama kwa kuwa kitasambaa nchi nzima kufikia 2020. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Serikali itaendelea kusanifu na kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara iweze kuleta mabadiliko ya utendaji. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
CHADEMA imedai madiwani wanaojiuzulu hushawishiwa kwa rushwa na ahadi ya ajira kutoka kwa viongozi wa Serikali wa Arumeru. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Serikali itaendelea kupambana na waharibifu wa mazingira na majangili wanaotumia mbinu, mikakati kuwaua wanyama ktk hifadhi. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Mama mwenye asili ya Z'bar amehukumiwa kifungo cha miaka 2 na nusu jela Uingereza kwa kudanganya amekufa ili apate pound 140,000. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Watu wasiojulikana wamechoma moto ofisi ya @ccm_tanzania tawi la Mshonzini, Mafia na kuteketeza vitu mbalimbali vilivyokuwemo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Wakazi wa Tabora wameshauriwa kuweka akiba ya kutosha ya chakula kabla hawajaamua kuuza mahindi yao ili kuepuka baa la njaa. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Vijana wa Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara na kiuchumi ktk nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Taifa halitopokea misaada yenye masharti ambayo haiendani na mila na desturi za Mtanzania. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa ametaka mikataba ya watoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa (JNIA) ipitiwe upya. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Wakili anayemtetea Harbinder Sethi ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa huyo anaumwa na hali yake ni mbaya akikosa usingizi kwa wiki 4. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
TAKUKURU inawashikilia Diwani wa Msigani (CHADEMA) na Mrasimu Ramani wa Manispaa ya Ubungo wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Waziri wa Habari Dkt. Mwakyembe ameunda Kamati maalumu na kuipa siku saba kuchunguza mkataba kati ya kampuni ya StarTimes na TBC. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 15, 2017
Mtanzania aliyewahi kuweka rehani gari lake kumsadia kijana ada ya Shule!!!!