Serikali imewaonya Watumishi wa Umma ambao wanapokea na kuzitoa siri za Serikali kisha kuzisambaza katika mitandao ya kijamii ikisema hilo ni kosa kubwa na adhabu yake ni zaidi ya miaka 20 jela kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amewaonya Watumishi wa Umma wanaopokea taarifa za serikali kinyume na sheria wazifute pamoja na kwamba kutaka kuonekana wa kwanza kusambaza taarifa.
>>>”Sisemi kwa vitisho lakini Serikali inawafatilia Maofisa na Watumishi waliovujisha taarifa za watu wenye vyeti vyenye utata kwani hao ndio wenye password na ndio walioingia kwenye mfumo uliokuwa na tangazo, mtashuhudia tu kitakachowapata muda si mrefu.”
Kwa upande mwingine, Waziri Kairuki amewataka Watumishi kufanya kazi kwa kufuata maadili mema ili kuwa mfano wa kuigwa kwa wengine, pamoja na kuwa wabunifu na waadilifu na kutofanya kazi kwa mazoea akiwataka pia kuwahudumia Watanzania kwa staha bila kujali vyama, dini na hali zao za kipato.
Ukitaka kuona mwanzo mwisho alivyozungumza bonyeza play kwenye hii video hapa chini
MAAJABU: Mtu kazikwa alafu siku 3 baadae kapiga simu, mkanda mzima upo ukiplay hapa chini
VIDEO: Lissu alivyogoma kutoka Mahakamani ili asikamatwe na Polisi, tazama kwenye hii video hapa chini