Baada ya hivi karibuni Sheria mpya ijulikanayo kama The Written Laws (Miscellaneous Amendment) Act, 2017 ilipitishwa na ambayo imeanza kutumika rasmi July 7, 2017, kumefanyika marekebisho kadhaa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amekutana na Waandishi wa Habari na kutolea ufafanuzi juu ya marekebisho hayo akisema>>>”Kufuatia kupitishwa kwa Sheria Mpya ijulikanayo kama The Written Laws ‘Miscellaneous Amendments’ Act, 2017 iliyoanza kutumika July 7, 2017 kumefanyika marekebisho kadhaa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.” – Prof. James Mdoe.
Aidha, Prof Mdoe ameyataja marekebisho makubwa yaliyofanywa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kuwa ni pamoja na;
1: Kuanzishwa kwa Tume ya Madini (Mining Commision)
2: Kufutwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (Tanzania Mineral Audit Agency – TMAA)
3: Kuongezeka kwa malipo ya Mrabaha kutoka 4% kwa madini ya Metali (Dhahabu, Shaba, Fedha n.k.) hadi 6%.
4: Kuongezeka kwa malipo ya Mrabaha kutoka 5% kwa madini ya Almasi na vito (Tanzanite, Ruby, Garnets n.k.) hadi 6%.
Tazama mengi zaidi aliyoyatolea ufafanuzi Prof. Mdoe PLAY kwenye VIDEO hii…
FULL VIDEO: Fatma Karume Wakili wa Lissu aongea kinachoendelea…tazama kwa kuplay video hii!!!