Kwenye utoaji wa tuzo hii uliofanyika Lagos Nigeria, midfielder wa Ivory Coast… mkali ambae anaichezea Manchester City baada ya ushindi wa hii tuzo kwa mara ya tatu amesema ‘nampongeza kaka yangu Obi Mikel ambae anastahili pia, najivunia na nimefurahi kuwa mshindi leo’
Gazeti la The Gurdian limeandika mkali huyu saa 24 baada ya kuifungia Manchester City kwenye mechi iliyokua na ushindi wa 6-0 dhidi ya Westham, ametangazwa mshindi huku akiongoza pia kwenye kura nyingi zilizopigwa na makocha wa timu mbalimbali za taifa Afrika.
Kwenye tuzo hizi naambiwa nafasi ya pili imeshikwa na mkali wa Chelsea Mikel Obi na ya tatu imechukuliwa na Didier Drogba.
Kwenye historia ya hizi tuzo Abedi Pele wa Ghana aliwahi kushinda hii tuzo mara tatu kuanzia mwaka 1991 mpaka 1993 wakati Samuel Eto’o wa Cameroon aliichukua hii tuzo kuanzia mwaka 2003 mpaka mwaka 2005 na tena akaichukua mwaka 2010.