Bado hatua ya mtoano ya michuano ya Ndondo Cup 2017 inaendelea katika uwanja wa Kinesi katika mtaa wa Victor Wanyama, leo July 22 hatua ya mtoano ya 16 bora ya Ndondo Cup imeendelea kwa kuzikutanisha timu za Boom FC dhidi ya Keko Furnitures.
Mchezo kati ya Boom FC na Keko Furnitures uliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, hivyo mikwaju ya penati ikabidi kupigwa ili kuamua mshindi wa mchezo huo atakayeingia robo fainali.
Hatua ya mikwaju ya penati kati ya Boom FC dhidi ya Keko Furnitures ilimalizika kwa Keko Furnitures kuitoa Boom FC kwa mikwaju ya penati 2-1, mchezo wa leo haukuishiwa vituko na mbwembwe kutoka kwa mashabiki wa pande zote mbili, unaweza kuangalia video mashabiki wakati wa game hapo chini.
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)