Ni wiki kadhaa zimepita toka tusikie zile stori kuwa shirikisho la soka Tanzania TFF limewatekelekeza vijana 22 wa timu ya Serengeti Boys waliyopo katika shule ya Alliance Sports Academy ya Mwanza.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri mmiliki wa shule ya Alliance ya jiji Mwanza James Bwire alikuwa na makubaliano na TFF kuhusu vijana 22 waliyochujwa kuingia katika shule ya Alliance ambao ndio wanatarajiwa kuunda timu ijayo ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys.
Leo AyoTV imempata katika exclusive interview mmilikiwa wa shule ya Alliance Sports Academy ya Mwanza James Bwire, wamefikia wapi na TFF kuhusu madai ya vijana hao kutelekezwa? kwa wasio fahamu walikuwa na makubaliano gani kati yake na TFF kuhusu vijana hao 22 waliyopo shuleni kwake?
“Naomba niseme tu hapo awali kulikuwepo kidogo na sintofahamu ya hapa na pale lakini nashukuru sana, baada ya game nilipata nafasi ya kuonana na kuzungumza na kaimu katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi na makamu mwenyekiti tumezungumza na kuweka mambo vizuri” >>> James Bwire
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)