Rais Magufuli leo July 25, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alikuwa katika Mkoa wa Singida alikozindua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa km 89.3 ambapo mbali na kufanya uzinduzi huo alipata nafasi ya kuhutubia wananchi.
Katika hotuba yake kwa Wananchi wa Itigi, Singida, Rais Magufuli alitoa agizo kwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads kupitia upya makubaliano ya ujenzi wa barabara na Mkandarasi.
Rais Magufuli alisema:>>>”Tunaanza na kilometa 57, quotation za bei ninaziona ni Bilioni 104, haiwezekani. Kwa maana nyingine kilometa moja inajengwa kwa zaidi ya Bilioni 1. Nataka Tanroads, Mtendaji Mkuu uko hapa uzipitie hizo upya.
“Wakati mnapatana na Mkandarasi, hizo mulizozipanga Bilioni 104, akikubali huyo anayetaka kujenga mumuongeze eneo, sio kilometa 57, ziendelee mbele zaidi. Akikataa punguzeni hizo hela mumpe thamani inayolingana na kilometa 57 zingine mtangaze kuendelea mbele. Nataka pawe na matumizi bora ya fedha.
“Nilipokuwa Waziri wa Ujenzi nilimfukuza Mtendaji Mkuu. Niliporudishwa tu Wizara ya Ujenzi aliondoka baada ya siku Tatu. Ni kwa sababu ya matumizi ya ovyo ya quotation katika ujenzi wa barabara.” – Rais Magufuli.
Kufahamu zaidi alichokisema JPM bonyeza playa hapa chini kutazama….
“Matatizo yaliyo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM