Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha, Innocent Mosha na Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Longido Vicent leo July 26, 2017 wamefikishwa tena Mahakamani na kesi yao imeahirishwa hadi August 24 watakaposomewa maelezo ya awali
Aidha, Hakimu Jasmin Abdul amesema kesi hiyo itapangiwa Hakimu wa kuisikiliza kwa kuwa tayari upelelezi umeshakamilika.
Tunakumbuka ajali ya basi la Wanafunzi wa Lucky Vincent iliyotokea Karatu, Arusha na kuua 32 na kuacha Majeruhi watatu ambao wanatibiwa kwenye Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa, Marekani huku Mmiliki wa shule hiyo na Makamu Mkuu wa Shule wakishikiliwa na Polisi wakikabiliwa na mashtaka matano.
Mashtaka wanayokabiliwa nayo ni pamoja na Mmiliki kuruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.
Mashtaka mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja Kaimu Mkuu wa Shule kuratibu safari na kuruhusu gari kuzidisha abiria.
ULIKOSA??? “Wabunge hatufanyi tuliyowaahidi Wananchi” – Dr. Tulia