Wengi tumeanza kumfahamu kupitia nafasi yake aliyonayo kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ila amekubali kukaa na millardayo.com na kuongelea upande wake wa pili,tumezoea kumsikia tu bungeni akiwa kazini ila hajawahi kupata nafasi kama hii aeleze yake ya moyoni.Anakwambia ….
‘Kwa kweli mimi ni aina ya mtu ambaye sipendagi sana madaraka makubwa mimi napenda sana kuwa mtu wa kawaida hapa wa katikati ,hata hapa kwenye unaibu spika nafurahi kweli maana kumbuka naibu spika mimi ni msaidizi wa spika kwa hiyo hata moto ukiwaka sana utamuwakia mama makinda napata joto kwa sababu msaidizi wake,sina ndoto kubwa za kwenda wapi wala wapi’
‘Naupenda sana mkoa wa Dodoma una changamoto kubwa sana ningependa sana kushiriki kuzifanyia kazi nimejaribu kushiriki kuzifanyia kazi kama mwanasiasa lakini naota kama katiba yetu itakuja kufanana kama ya Kenya,ile ya Kenya wakuu wa mikoa wanachaguliwa na wananchi wanaitwa Gavana’
‘Katiba yetu ya Tanzania kama itatokea imetoa nafasi za Ugavana wa mkoa unagombewa sio wa kuteuliwa mimi nitagombea Ugavana wa kuwa Gavana mkoa wa Dodoma ili kujaribu kuubadilisha mkoa wa Dodoma katika ndoto zangu kuweza kuibadilisha na kuwasaidia hawa ndugu zangu kuwatoa hapa walipo na kuwasukuma mbele zaidi kwakweli mi binafsi ndoto yangu ni hiyo’
‘Hapa zipo changamoto za kutosha kabisa kuna umaskini wa kutosha watu wa Dodoma ndo wanadharaurika kwa kuonekana Ombaomba nchi nzima nikipata fursa hiyo nadhani naweza kuibadili hiyo hali kwa hiyo ni moja ya ndoto zangu inategemea kama katiba mpya itatoa nafasi kama hiyo na wananchi wa Dodoma wakaniamini basi nadhan naweza kushirikiana nao kuibadili hii hali ya Ombaomba kuwa tegemezi wa chakula kila mwaka Chakula cha Serikali,Chakula cha Njaa lazima tuhakikishe vijana wa Dodoma wanasoma’
‘Niliwahi kutembelea jimbo moja kule India ni jimbo kame kama ilivyo Dodoma lakini wana maendeleo makubwa sana kwa sababu wao walichofanya waliwekeza kwenye elimu,kwa hiyo hilo jimbo linatoa madaktari,manesi dunia nzima unaweza ukatengeneza ukajenga vyuo’
‘Watu wa mkoa wa Dodoma badala ya kutegemea kilimo kisichotabirika wanaweza wakatoa wataalam wakatoa manesi wakatoa madaktari wa nchi nzima hapa wakatoa mabwana kilimo wa nchi nzima yaani fursa ni nyingi sana ambazo ukiwa na nafasi za utendaji tofauti na nafasi ya uwakilishi niliyonayo hivi sasa’
‘Nafasi niliyonayo sasa hivi ni kuwasemea wananchi lakini kutenda ni ngumu lakini nafasi ninayoisemea hiyo ni ya kutenda unapokuwa Gavana unatekeleza unapanga mambo unahakikisha yanatekelezeka’.