Kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 28, 2017 issue nyingi zimechambuliwa ambapo miongoni mwao ni issue ya Afisa Mtendaji wa Kijiji kujinyonga hadi kufa akihofia kuhojiwa na Polisi baada ya kupotea msichana.
millardayo.com imezikusanya tweets zote zilizohusu uchambuzi wa Magazeti ya leo kutoka kwenye twitter yangu @millardayo.
Mahakama ya Mkoa Mwera imeahirisha kwa mara ya 5 kutoa hukumu kwa Idrisa Ali Idrisa anayetuhumiwa kudhalilisha watoto kijinsia. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Mkazi wa Ipagala, Dodoma Charles Kalinga amenusurika kifo baada kupigwa na wananchi akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa Form 4. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Kamati ya Tume ya Utumishi wa Umma na Walimu (TSC) wilayani Nyang'hwale, Geita imewafukuza kazi walimu 7 kwa kosa la utoro. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Serikali mkoani Arusha imewataka viongozi wa dini kutojiingiza kwenye siasa badala yake waendelee kuimarisha amani na mshikamano. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
DC Chunya, Mbeya amemsimamisha kazi mtumishi wa Hospitali ya Wilaya kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 15,000. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Mtu mmoja amefariki na wengie 13 kujeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mpanda baada ya basi walilokuwa wanasafiria kupinduka, Katavi. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Spika Job Ndugai amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Afrika. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Wanachama wa CCM wametakiwa kutowaonea haya viongozi wasiokuwa mstari wa mbele kushirikiana na wananchi kuharakisha maendeleo. #Majira.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Serikali imesema itavichukua viwanda visivyoendelezwa 54 kati ya 156 vilivyobinafsishwa kati ya mwaka 1992 hadi 2004. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Watumishi 29, wengi wakiwa madereva na wahudumu wa Ofisi za TAMISEMI, wamefukuzwa kazi kutokana na kuwa na elimu ya Darasa la 7. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Mapacha walioungana wamefanyiwa vipimo kupitia mashine ya uchunguzi wa magonjwa (MRI) kuona kama upo uwezekano wa kuwatenganisha. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kiraracha, Moshi amejiua kwa kujinyonga akihofia kuhojiwa na Polisi kwa tukio la kupotea msichana. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Mbunge wa Hanan'g Dr Mary Nagu (CCM) amesema hajawahi kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa agizo la DC wa Hanan'g. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Waziri Jenista Mhagama ametoa siku 30 kwa waajiri ambao hawajasajili, kujisajili katika Mfumo wa Fidia wa Wafanyakazi (WCF), #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
TAKUKURU Mara imemfikisha Mahakamani Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Musoma kwa kujipatia fedha kwa udanganyifu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Baada ya Rais Magufuli kusema ataifungia kampuni ya Barrick Gold Mine, uongozi wa kampuni hiyo unatarajia kuja wiki ijayo. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi, Mbunge Tundu Lissu ameahidi kutonyamaza. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ameutaarifu umma akiuelezea uamuzi uliofanywa na Prof. Lipumba, Bunge na NEC kuwa ni hujuma. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangza majina mapya 8 kuchukua nafasi za Wabunge waliofukuzwa uanachama Chama cha Wananchi CUF. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Polisi wenye silaha Kilwa, Lindi wanadaiwa kuvamia msikiti, kuwapiga risasi Masheikh 10 na kusababisha kifo cha mmoja wao. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Rais Magufuli amemuagiza RC Morogoro kuwaruhusu wafanyabiashara ndogo ndogo kuingia ndani ya Kituo kipya cha mabasi, Msamvu. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu hairidhishwi na juhudi zinazofanywa na raia kulalamika badala ya kufanya shughuli za maendeleo. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Wanawake wenye nafasi mbalimbali za uongozi wameombwa kushiriki mapambano dhidi ya ukeketeji ambao sasa hufanywa kwa watoto wachanga. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutanguliza mbele uzalendo katika mambo wayaandikayo kuhakikisha yanaitangaza nchi. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
Rais Magufuli amewataka waliobinafsishiwa viwanda mbalimbali mkoani Morogoro kuvirejesha serikalini kama wameshindwa kuviendeleza. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 28, 2017
VIDEO: Tundu Lissu afunguka ishu ya kutaka kupimwa mkojo na mengine…bonyeza PLAY kutazama!!!
ULIPITWA na hii VIDEO? Alichozungumza Wakili Fatma Karume baada ya Tundu Lissu kupewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu…bonyeza PLAY kutazama!!