Mmoja kati ya watu waliyohudhuria mchezo wa pili wa robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017 kati ya Goms United dhidi ya Mlalakuwa Rangers ni waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba.
Waziri Mwigulu alifika kushuhudia mchezo wa robo fainali hiyo ambayo Goms United walimaliza kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, baada ya hapo waziri Mwigulu alivutiwa na uwezo wa mchezaji wa Goms na kumuomba Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga wachukue mawasiliano yake, inawezekana wakamchukua?
“Kwanza timu zote walikuwa wanacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha kuwa wanatafuta ushindi huku wakihakikisha hawaruhusu goli kuingia kwao , tumeona pia waliyofungwa baada ya kuingia lile goli hawakupoteana hiyo ni sifa kubwa katika mpira” >>>Mwigulu
VIDEO: Vituko vya team Shilawadu wakiifunga Leo Tena mbele ya waziri Mwigulu