Majadiliano kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Magufuli na Wawakilishi kutoka Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini yameanza leo July 31, 2017 Dar es Salaam.
Kamati hiyo inaongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi wakati Kamati ya Barrick Gold Corporation inaongozwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu Richard Williams.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa majadiliano hayo Prof. Kabudi amesema Kamati yake imejipanga vizuri kujadiliana na Barrick Gold Corporation juu ya madai ya Tanzania katika biashara ya madini na itahakikisha inasimamia maslahi ya Tanzania ipasavyo.
Naye Richard Williams ameshukuru kuwepo kwa majadiliano hayo akisema Kampuni ya Barrick Gold Corporation imeyapokea madai ya Tanzania kwa mtazamo chanya na ipo tayari kujadiliana na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote mbili.
ULIPITWA? Ripoti ya Pili ilivyomuumiza Rais Magufuli…tazama hapa kila kitu kwa kuplay kwenye hii video!!!!