Baada ya kumalizika kwa michezo ya robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017 na kuzishuhudia timu za Misosi FC ya Tandale, Goms United ya Gongo la Mboto, Kibada One ya Kigamboni na Keko Furniture ya Keko zikifuzu hatua ya nusu fainali.
Usiku wa July 31 droo ya nusu fainali ilichezeshwa na kushuhudia timu za Keko ikipangwa na Misosi FC wakati Kibada One wakipangwa kukutana nusu fainali Goms United. Michezo ya nusu fainali imesogezwa mbele hadi August 9 na 10 ili kupisha shughuli ya kitaifa ya uzinduaji wa bomba la mafuta.
Kabla ya droo, team Leo Tena ikiongozwa na Husna imetoa zawadi ya Tsh 300,000 kwa club ya Mlalakuwa Rangers kama kifuta jasho baada ya kuondolewa katika michuano hiyo na kuahidi kumfanyia tafrija ya kumuaga golikipa wao ambaye anaenda Mbeya City.
Baada ya droo ya nusu fainali iliyofanyika leo MisosiFC vs Keko Furniture na nusu fainali ya pilu Goms UTD vs Kibada One #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/z3KiVjuoks
— millard ayo (@millardayo) July 31, 2017
VIDEO: Vituko vya team Shilawadu wakiifunga Leo Tena mbele ya waziri Mwigulu