Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania ‘TPSF’ juu ya athari zitokanazo na hatua ya Serikali kuhamisha fedha zake kutoka Taasisi binafsi za kifedha kwenda Benki Kuu ‘BoT’ umeonesha kuyumba kifedha kwa sekta ya mabenki nchini.
Wakati wa uchambuzi wa utafiti huo wadau wa uchumi wameishauri Serikali kushirikisha wadau mbalimbali katika kutoa maoni kabla ya kufanya maamuzi au kutengeneza sera za uchumi ili kuangalia faida na hasara zake.
Miongoni mwa Wachambuzi ambao wameielezea hali hiyo ni pamoja na Prof. Honest Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye amesema sekta ya mabenki binafsi imetikisika kutokana na hatua ya Serikali kuhamisha fedha zake na kuzipeleka Bank Kuu.
>>>”Utafiti unatizama baada ya Serikali kuondoa fedha zake katika Sekta ya Mabenki binafsi na kuziweka Bank Kuu. Utafiti huu uliofanywa na TPSF umeonesha kwamba kwa kiasi fulani imefanya Mabenki kutikisika na kupata matatizo ya fedha.” – Prof. Ngowi
ULIPITWA? Serikali imewajibu wanaosema uchumi wa Nchi umeporomoka…tazama kwenye video hapa chini!!!