Siku kadhaa zilizopita zilienea taarifa zilizodai kuwa Mwigizaji staa wa Vichekesho Bongo Amri Athumani maarufu kama King Majuto amefariki taarifa ambazo baadaye zilibainika kuwa hazikuwa za kweli.
Ayo TV na millardayo.com zilifunga safari hadi Tanga nyumbani kwa Mzee Majuto na kufanya naye mahojiano mbalimbali yakiwemo taarifa hizo za kuzushiwa kifo mara kwa mara.
>>>”Nimeshazushiwa mara tano hadi sasa kwamba nimefariki, mara ya kwanza nilipokwenda kuhiji Makka wakazusha nimefariki. Ki ukweli haya mambo hayapendezi hata kidogo.
“Mimi ina watu kama vile ndugu zangu ambao wengine wanakaa mbali sasa wanapopokea taarifa kama hizi, sio ustaarabu.
Alizipata wapi taarifa za hivi karibuni kwamba amefariki?>>>”Kwanza namchukia mwandishi mmoja wa gazeti nimelisahau aliniandika kuwa naumwa na HERNIA tukalaumiana sana na wakati huo hata sikuwa nikiumwa chochote. Kama alikuwa mchawi wangu hazikupita hata siku kumi wakati natoka Kenya nikaumwa kweli HERNIA hivyo nikakimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji.
“Unajua wakati unafanyiwa upasuaji unakuwa bado huna fahamu sasa kuna mtu akapiga picha wakati nimelala pale wakatengeneza na kusema nimekufa. Mimi kwa sasa ni mzima wa afya na binadamu ana mambo mawili…kuishi akiwa mzima au na maradhi.
“Najua hata mimi ni lazima nife kwa maana hata babu yangu hayupo, mama yangu hayupo na hata Rais wangu niliyekuwa nikimpenda sana Nyerere hayupo. Kwa hiyo, ni lazima tuondoke.” –Mzee Majuto.
ULIPITWA? Taarifa za kuzushiwa kifo zimemfikia King Majuto, katuma Ujumbe ‘Sote tutakufa’…tazama kwenye video hii!!!