Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya Wema Sepetu ya kutaka kielelezo cha sampuli ya mkojo wake kisipokelewe mahakamani. Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema anakubaliana na upande wa mashtaka kwamba kielelezo cha mkojo wa Wema kipokelewe na Mahakama kama sehemu ya ushahidi.
Pingamizi la Wema kupitia wakili wake Kibatala ni kwamba ripoti iliyowasilishwa na Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu, Elias Mlima ya kwamba mkojo wa Wema una chembe chembe za dawa za kulevya aina ya Bangi haikukidhi matakwa ya kisheria. Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 16/2017.
Wema Sepetu na wengine wawili wanakabiliwa na makosa ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi Februari mwaka huu .