Baada ya matarajio ya muda mrefu kwa mashabiki wa soka wa Dar es Salaam Young Africans kuhusu kunasa saini ya beki wa pembeni wa Azam FC Gadiel Michael kuchelewa kwa madai kuwa Azam FC walichelewa kujibu barua yao, hivi karibu zimetoka taarifa kuwa Azam FC tayari imeshawajibu Yanga kwa barua lakini haikuweka wazi imewajibu nini?
Leo tumempata katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa azungumzie ishu hiyo, ni kweli Azam FC wamejibu barua yao? na vipi wamefikia wapi sasa kuhusiana dili la kumpata Gadiel Michael ambaye inaaminika tayari alishasaini Yanga
“Ni kweli kama nilivyosema kulikuwa kuna taarifa ambazo sio za ukweli sana pengine zilikuja kwa ajili ya watu kutaka kupata chochote lakini baada ya kumsaini tunaambiwa mkataba wake unamalizika hadi December tuliwaomba Azam FC lakini wametuandikia barua ya kutaka ada kubwa” >>> Boniface Mkwasa
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)