Siku moja imepita toka club ya Dar es Salaam Young Africans kupitia kwa katibu Mkuu wake Charles Boniface Mkwasa kuilalamikia club ya Azam FC kuwa inawabania kumpata mchezaji Gandiel Michael wakati Simba huwa wanasajili wachezaji kutoka Azam FC bila pingamizi.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Azam Jafari Iddi Maganga ameweka wazi Azam FC kubadili mawazo na kuamua kuwapunguzia ada ya uhamisho kutoka kiasi cha awali walichokitaka na sasa wamewaambia watoe nusu ya ile hela ili wamsajili Gadiel.
“Leo Azam FC walikuwa na mazungumzo na Yanga kuhusiana na mchezaji Gadiel Michael, kifupi Yanga walikuwa wanamuhitaji Gadiel Michael lakini tulikuwa hatujapata muafaka, Yanga leo walikuja kupitia kwa mwenyekiti wao wa usajili na tumeafikiana walipe nusu ya dau la awali” >>> Jafari Iddi
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)