Hii ni habari kubwa sana ambayo imebeba vichwa vingi vya magazeti mengi leo,ni kuhusu mtafaruku uliosababisha mauaji kati ya wakulima na wafugaji huko wilayani Kiteto katika mkoa wa Manyara 107.3[Clouds Fm]Gerald Hando wa Power Breakfast ameongea na mkuu wa wilaya Kiteto Bi.Martha Wambura hiki ndicho alichokisema.
‘Kwa bahati mbaya ni mgogoro ule ule unaendelea kwa namna ambavyo wanajaribu kupambana kwa jamii hizi mbili za wakulima na wafugaji kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kwenye hifadhi hii ya jamii nadhani ni watu wameamua kujichukulia sheria mkononi wameenda huko msituni wakijaribu kuwaondoa wale wakulima ambao kila mara wanambiwa watoke lakini hawatoki’
‘Hali halisi kwa sasa imedhibitiwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa akiwemo mwenyekiti mwenyewe mkuu wa mkoa tangu jana wanajaribu kuhakikisha amani inarudi mahali pake na tunaidhibiti hali hii na kutia hatiani wahusika’
Hizi ni dakika tatu za mahojiano kati ya Gerald Hando na Mkuu wa wilaya ya Kiteto Bi.Martha Wambura akielezea hali ilivyo kwa sasa.