Ni muda mrefu sasa headlines za Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF zimekuwa zikiongoza kwenye mitandao mbalimbali.
Sasa leo tunazihesabu siku Nne pekee kuelekea Uchaguzi huo ambao utafanyika Jumamosi August 12, 2017 Dodoma ambapo Wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza Kampeni na miongoni mwao ni Shija Richard Shija amezindua rasmi kampeni zake.
Shija anayegombea nafasi ya Urais wa TFF ameahidi kutekeleza mikakati ya muda mrefu na mfupi kuhakikisha analifanyia mageuzi soka la Tanzania ili liweze kuendelea mbele zaidia Miguu Tanzania kwa kuhakikisha anatekeleza sera na mikakati ya muda mrefu na muda mfupi.
Mikakati ya muda mrefu ni pamoja na miundombinu ya kutambua vipaji vya mpira wa miguu na miundombinu ya kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu huku baadhi ya mikakati ya muda mfupi ikijumuisha kusimamia utekelezaji wa Azimio la Bagamoyo katika maeneo makuu manne ambayo ni Taasisi za Mpira na Utawala, Ufundi, Upatikanaji wa vifaa bora na Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Aidha ameahidi kusimamia uadilifu na utawala bora katika uendeshaji wa mpira, kupeleka rasilimali fedha mikoani, kuongeza ari ya kushiriki na kuwekeza kwenye michezo, kuendeleza miundombinu na kuhamasisha udhamini katika mpira wa miguu na kusimamia weledi.
ULIPITWA? Mabadiliko yaliofanywa katika kikao baada ya kamati kusitisha uchaguzi wa TFF…tazama kwenye video hii!!!
Tazama hapa TFF baada ya Yanga kutaka iombwe radhi kwa kutopewa mwaliko!!!
ULIPITWA na hii Sababu iliyofanya uchaguzi Mkuu wa TFF kusitishwa? Tazama kwenye video hii!!