Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo August 8, 2017 amenusuria kwa mara nyingine jaribio la kuondolewa madarakani baada ya Bunge la nchi hiyo kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani naye.
Kufuatia mjadala mrefu na mchakato wa kupiga kura uliodumu kwa saa mbili, Wabunge 198 walipiga kura kupinga azimio la Democratic Alliance ambao walipiga kura 177 wakionesha kutokuwa na imani naye.
Aidha, Wabunge 30 wa Chama tawala cha ANC walipiga kura kutaka Zuma aondolewe ambapo ili kuondolewa madarakani zilihitajika kura 201.
Spika wa Bunge la Afrika Kusini Baleka Mbete alitangaza Jumatatu kuwa kura zitapigwa kwa siri kwa mara ya kwanza tofauti mara kadhaa zilizopita ambazo kura za kutokuwa na imani na Zuma zipigwa kwa njia ya wazi.
Rais Zuma amenusurika jaribio la kuondolewa madarakani baada ya kupata kura 198 dhidi ya 177 zilizosema aondoke. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/YP530WkHX6
— millardayo (@millardayo) August 8, 2017
Kipo hapa alichoongea Rais Magufuli baada ya Rais Zuma kuwasili Tanzania…tazama kwa kuplay!!!!