Kwenye ulimwengu wa sasa mtu kuweza kuishi zaidi ya miaka 80 inaaminika kuwa jambo kubwa na la kifahari sana, na hii inatokana na ripoti mbalimbali duniani zinazoonesha kuwa wastani wa masiha ya watu unapungua siku hadi siku kutokana na sababu mbalimbali.
Moja kati ya ripoti hizo ni ‘ripoti ya furaha duniani 2017’ kwa sababu hizo mbalimbali life span imeshuka hadi kufiki wastani wa miaka 71.
Wataalamu mbalimbali wamefanya utafiti kutokana na ripoti huyo kugundua nchi tano duniani ambazo watu wake huishi miaka mingi zaidi kujua sababu za jambo hili. Ayo TV na millardayo.com inakuletea orodha hiyo
5. Uswisi
Namba nne inachukuliwa na Uswisi ambapo wanaume wa nchi hii huishi sana kuliko mataifa yote duniani kwa kufikisha wastani wa miaka 81. Hii ikiwa nchi tajiri sana kuliko nchi zote barani Ulaya mifumo ya afya bora na usalama wa watu binafsi umesabisha mafanikio haya ya maisha marefu kwa watu wake.
Raia wa Uswis wanaelezewa kuwa watumiaji wakuu wa maziwa na jibini yaani ‘cheese’ ambavyo huwapa afya zaidi ya kuishi miaka mingi.
Mwanasayansi wa Chakula nchini Denmark alifanya utafiti kwa kupima mkojo wa watu 15 ambao walikuwa wamekula chakula chenye aidha jibini, maziwa au karanga na kugundua kuwa wale waliokuwa wamekula jibini wana acid ambayo inajulikana kama butyric ambayo inahusishwa na kupungua kwa cholestrol mwilini yaani lehemu au kwa namna ya kueleweka kirahisi ni mafuta mwalini jambo ambalo linapunguza hatari za magonjwa ya moyo.
Maziwa kwa upande wake inaelezwa kuwa inapungunza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi kwa asilimia 15 hadi 20.
4. Hispania
Namba nne inashikwa na Hispania ambapo watu wa nchi hii huishi miaka hadi 82.8 kwa wastani. Mafanikio yao makubwa kwenye suala hili pia yanatokana na vyakula wanavyokula na maisha wanayoishi yaani lifestyle. Watu wa Hispania hutumia kwa wingi mafuta ya mzeituni, mboga za majani and mvinyo yaani ‘wine’.
Mafuta ya mzeituni yaani olive oil yanatajwa na wanasayansi kuwa na utajiri mkubwa wa virutubisho ambavyo hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kisukari, saratani na mengineyo, lakini pia ni tiba bora ngozi inayozeeka na magonjwa ya kuzeesha mwili.
Mboga za majani zenyewe zinaelezwa kuwa na virutubisho ambavyo husafisha na kupambana na sumu mwilini. Wataalamu wanaeleza kuwa kula bakuli moja la mboga za majani hupunguza hatari ya kufa ndani ya miaka minne kwa nusu kwa matu wenye umri wa kati tofauti na wasiokula mboga za majani.
Kwa upande wa mvinyo yaani wine miaka kadhaa iliyopita wataalamu walieleza kuwa nusu glass ya wine kwa sikuhuweza kuongeza miaka 5 ya maisha.
3. Japani
Kiwango cha wastani cha maisha kwa watu wa nchi hii ni miaka 83. Hii inaelezwa kuchangiwa na hii inachangiwa na vyakula vyao vya asili wanavyokula. Vyakula hivi ni pamoja na viazi vitamu na kiasi kidogo cha samaki.
Wataalamu wanaeleza kuwa viazi vitamu husaidia sana katika kuweka sawa viwango vya sukari mwilini. Inaelezwa pia kuwa viazi vitamu huupa mwili asilimia 100 ya vitamin A, asilimia 37 vitamin C, 16 % ya vitamin B6 na 18% ya madini potasium. Pia huwa na kiwango kidogo cha madini aina ya calcium, chuma, phosporus, folate na zinki.
Samaki kwa upande wake huwa na virutubisho aina ya Omega 3 fatty acid ambavyo hulinda moyo na kupunguza athari ya magonjwa ya mshtuko wa moyo na kiharusi. Utafiti huu ulifanywa miaka ya hivi karibuni na Shule ya Havard ya Afya ya Jamii katika chuo kikuu cha Washngton Marekani.
2. Singapore
Singapore ni nchi ya tatu kwenye orodha hii na watu wake huishi hadi kufikia miaka 83.1 na nchi hii ndio yenye kiwango kidogo cha vifo vya wamama wajawazito na watoto, na hii ni kutokana na mifumo yake bora ya utoaji wa huduma za afya nchi nzima.
1. Korea Kusini
Korea Kusini ndio nchi ya kwanza ambayo watu wake huishi maisha marefu zaidi duniani. Nchi hii huwa na watu wanaofikia umri wa miaka 90. Tofauti na kuwa na uchumi mkubwa na huduma bora za afya raia wake wanasifika kwa kula vyakula vya kuvundikwa yaani processed food. Vyakula hivi ni vile ambavyo havina cholesterol, huongeza kinga ya magonjwa mwilini na kuzuia magonjwa ya saratani.
Ulipitwa na hii? WEMA KURUDI CCM: “WAZEE WALIONGEA”