Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kupitia kwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Suzan Lyimo amedai baadhi ya masharti ya Mikopo ya Elimu ya Juu inaimarisha dhana ya ubaguzui na matabaka katika utoaji wa elimu ya juu nchini.
Lyimo amesema kuwa masharti hayo yanayomtaka muombaji wa mkopo kuwa chini ya miaka 30, kuomba mkopo akiwa amemaliza Kidato cha Sita au awe na sifa linganifu kama Diploma ndani ya miaka mitatu mpaka kipindi cha kuomba mkopo huo.
>>>”Tunapendekeza marekebisho ya masharti haya ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Tume Maalumu ambayo itaangalia changamoto katika mfumo wetu wa elimu kuanzia ngazi ya Awali hadi Chuo Kikuu. Tume hii pia iangalie jinsi tutavyoweza kugharamia Elimu ya Juu.” – Suzan Lyimo.
ULIKOSA?? CHADEMA wafunguka azimio jingine la Kamati Kuu…tazama kwenye hii video!