Ikiwa imepita takriban miezi minne tangu kupigwa marufuku utengenezaji, usambazaji, uuzaji na unywaji wa pombe ilifungashwa kwenye mifuko ya plastiki maarufu kama ‘viroba’ Serikali imesisitiza kuwa haina nia ya kuirudisha sokoni badala yake wafanyabiashara wakaiuze nje ya mipaka ya Tanzania.
Akiwa katika ziara ya kushtukiza katika ghala la Kampuni ya usambazaji wa vinywaji aina ya viroba, Thema, Kimara Temboni Dar es Salaam Waziri wa Mazingira January Makamba amesema pombe hizo hazitouzwa tena nchini badala yake Serikali itatoa vibali kwa wafanyabiashara ambao bado wana shehena kwenye maghala yao wakauze nje ya nchi.
>>>”Pombe yote ikusanywe kwenye maduka na magodauni ipelekwe kwa wazalishaji ili ama waifunge kwenye chupa au waiuze kwenye soko la nje lakini zuio bado liko palepale la kuzalisha, kusambaza, kuuza, kuingiza nchini pombe za viroba.” – January Makamba.
Tazama kila kitu kwenye video hii hapa chini!!!
ULIPITWA? Ripoti ya MCT kuhusu Uchunguzi wa uvamizi wa Clouds Media Group…tazama kwenye video hii hapa chini!!!