Baada ya Jeshi la Polisi na Maofisa Magereza kutumia nguvu kuwadhibiti wafuasi 13 wa Chama cha Wananchi CUF ambao waliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ayo TV na millardayo.com zimempata Wakili wa Utetezi Hashimu Bakari Mzirai kuzungumzia tukio hilo.
Wakili Mzirai alisema wakati Hakimu anaendelea kusikiliza kesi waliingia Askari na kuwakamata wanachama hao jambo ambalo amesema watafungua kesi dhidi ya watu waliotoa amri ya kukamatwa kwao.
Aidha, Wakili huyo alisema ili mtu akamatwe lazima awe ametenda kosa au kuwe na hati ya ukamataji kitu ambacho Askari hao hawakua nacho.
PROF. LIPUMBA TENA: Ni kuhusu Wabunge wapya walioteuliwa…tazama kwenye video hii!!!