Jukwaa la Uchumi Duniani ‘WEF’ limetoa list ya nchi ambazo hazina vyoo vya kutosha Afrika kulingana na uwiano wa watu huku ikizitaja nchi kadhaa za Afrika ambazo zina uwiano mdogo wa vyoo.
Katika list hiyo Tanzania imetajwa kushika nafasi ya Tisa huku ikielezwa kuwa karibu watu Bilioni 1.1 katika nchi zinazoendelea hujisaidia kwenye mashamba, misitu, vyanzo vya maji na maeneo ya wazi suala linaloongeza magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, homa ya ini, taifodi, kuhara na mengineyo.
Suala la watu kujisaidia ovyo hususani kwenye vyanzo vya maji linaripotiwa kuathiri zaidi wanawake ambao ndio watumiaji wakuu wa maji hayo katika shughuli zao za kila siku.