Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba alikutana na waandishi wa Habari Dodoma na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuliagiza Jeshi la zimamoto kuchunguza chanzo cha matukio ya moto yanayoendelea kutokea nchini likiwemo tukio la kuungua kwa soko la sido mkoani Mbeya…>>>”Haya ni matukio ya hatari ambayo yamekuwa yakitugharimu sana mara kwa mara hivyo naelekeza kamati za ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina kujua nini hasa vyanzo vya matukio haya ya mara kwa mara ili kuchukua tahadhali kwa maeneo mengine ”
“Nitumie nafasi hii kutoa pole kwa wananchi wa Mbeya na wafanyabiashara kwa ujumla waliokumbwa na tatizo hilo, sisi kama Serikali tutaendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kukabiliana na matatizo kama haya pindi yanapojitokeza” –Waziri Nchemba
“Zaidi nitoe lai kwa halamashauri ambapo taratibu za ujenzi zinafanyika, mar azote wanapofanya shughuli za ujenzi wahakikishe wanashirikiana na mamlaka ya zima moto ili kuweka kwenye mpangilio matarajio ya namna vifaa vya uokoaji vinavyoweza kupita punde yanapotokea matukio kama haya”-Waziri Nchemba
Zaidi na hiyo Waziri Nchemba ametoa onyo kwa watu wanaosajili line za simu kwa majina ya watu wengine kisha kufanya utapeli…>>>”Kumezuka kwa mara nyingine watu kufanya utapeli kwa njia za simu huku wakisajili line zao kwa majina ya watu wengine” –Waziri Nchemba
“Natoa onyo kwa watu wanaofanya michezo hiyo kuacha tabia hiyo mara moja na kwa wale watakaokiuka watakutana na mkono wa dola, naelekeza kwa vimbo vya dola kuwa pindi mnapowakamata wahalifu hao msiwafikishe kwenye kwenye mkono wa sheria kisirisiri… watangazeni ili na wengine wajifunze” -Waziri Nchemba
Full Video nimekuwekea hapa chini tayari…
Ester Bulaya kufungua kesi dhidi ya Wasira? Aomba ushauri Jimboni