Leo August 16, 2017 Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, ‘UVCCM’ kupitia kwa Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo, Daniel Zenda imetoa ufafanuzi kuhusu Umoja huo kuamua kutoa msaada kwa wanaojiunga na Vyuo kuomba Mikopo ya Elimu ya Juu akisema kuwa nia yao sio ya kichama bali kuwasaidia Watanzania.
Hivi karibuni UVCCM ilitangaza mpango wa kwasaidia Watanzania wanaotaka kuomba mkopo lakini mpango huo uliiibua maswali huku baadhi wakidai mpango huo ni ajenda ya kisiasa.
Daniel Zenda>>>”Watu wengi wanakosa mikopo ya Vyuo kwa sababu hawana uelewa wa kutosha katika kufanya maombi hayo ndio maana tumeamua kuwasaidia ili kuisapoti Serikali katika azma yake ya kutoa elimu kwa Watanzania.”
Madiwani wasababisha Meya aahirishe kikao…kisa?