Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga leo August 17, 2017 ameagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Siday Denis Lukumay akamatwe na kuwekwa rumande akidaiwa kumruhusu mwanafunzi Yuditha Mohammed kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
DC Mofuga ameeleza kuwa Mkuu huyo aliruhusu mwanafunzi kusoma akiwa mjamzito na kuendelea na masomo pia baada ya kujifungua huku kitabu cha mahudhurio akionekana kuhudhuria kama kawaida.
>>>”Anaruhusu mjamzito kusoma akiwa shuleni. Ameenda kujifungua bado mahudhurio yanaonesha bado alikuwa shuleni. Badala ya kutafuta wahalifu waliompa mimba mwanafunzi, yeye anamuweka shuleni.” – DC Mofuga.
DC Mbulu ameagiza Mkuu wa Siday Sec awekwe rumande akidaiwa kuruhusu mwanafunzi kuendelea na Shule baada ya kujifungua #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/j5mb7mplP0
— millardayo (@millardayo) August 17, 2017
ULIPITWA? Maamuzi ya DC Karagwe baada ya kupotea porini siku nzima…tazama kwenye video hii hapa chini!!!
ULIPITWA? Kilichofanya RC Kagera kumuweka ndani Afisa kwa saa 48…tazama kwenye hii video hapa chini!!!!