Moja ya mipango ya nchi nyingi Duniani ni Ulinzi ‘kujilinda’ ambapo nchini zimekuwa zikitenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na kuhakikisha wananchi husika wanaishi katika hali ya salama na amani.
Zipo nchi nyingi ambazo zinatajwa kuwa na majeshi imara ambayo huwa ngumu sana kuvamiwa na majeshi ya nchi nyingine kwa namna yoyote lakini siyo zote zinaweza kujilinda ambapo kwa mujibu wa mtandao wa howafrica.com zimetajwa nchi 10 ambazo haziwezi kuvamiwa kirahisi.
10. Iran
Nchi hii ya Jiografia ya milima mingi kama ilivyo Afghanistan inatajwa kuwa na Wanajeshi zaidi ya Laki Tano, Vifaru vya kivita 1,658 na Ndege za kivita 137. Iran pia ina mitandao wa ghala za silaha za nyuklia ndani ya ardhi ambavyo vinasemekana kuwa vya mita 500 katika kila mji wa nchi hii.
9. Bhutan
Ni nchi iliyo katika safu za milima ya Himalaya ikisemwa kuwa kikosi cha Jeshi la watu 6, 000 bila silaha wala Jeshi la Anga lakini inaripotiwa kuwa haijawahi kuvamiwa tangu miaka ya 1700 lakini hapakuwa na madhara makubwa yaliyotokea. Inapatika mita 300 kutoka usawa wa Bahari na nchi ya India inajihusisha na ulinzi wa nchi hii ndogo kwa kuwapatia silaha na mafunzo jeshi hilo.
8. Australia
Miongoni mwa mawazo mabaya ni kutaka kuivamia Australia ambayo inatajwa kuwa na majeshi imara. Japan iliwahi kuwa na mawazo ya kuivamia Australia wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia lakini ilitupilia mbali wazo baada ya kubaini hata wakiingia katika nchi hiyo 95% ya tatizo ambalo wangalipata lingalibaki hadi sasa.
7. Russia
Hii ni nchi kubwa kuliko zote duniani. Na sababu kubwa mbili za kutovamiwa ni jiografia yake ambayo ni milima mingi pamoja na hali yake ya hewa ambayo ni baridi sana kwa viwango vya theluji nzito.
6. Korea Kaskazini
Nchi hii ina zaidi ya wanajeshi Milioni Moja, Vifaru 4,200 na Helikopta 222 za vita jambo linalofanya kuwa na Jeshi kubwa kuliko yote katika Jumuiya ya Kujihami ya NATO tofauti na Marekani. Inasemekana pia kuwa na silaha za nyuklia zinazoweka kufika Korea Kusini, Japan na hata Pwani ya Magharibi ya Marekani.
5. Israel
Israel imepigana mara nyingi ndani ya miaka 69 lakini haijawahi kushindwa. Nchi hii ina vikosi vya Jeshi 1,760,000 na, ni wajibu wa kisheria kwa kila raia wake kuhudhuria mafunzo ya kijeshi – wanawake wakifanya mafunzo kwa miezi 24 na wanaume miezi 36. Hii inamaanisha karibu kila mwananchi wake anaweza kutumika wakati wa vita.
4. Canada
Canada sio wazuri na hawana huruma inapokuja suala la vita. Nchi hii ina jumla ya Wanajeshi 95,000 waliopewa mafunzo. Kama ilivyo kwa Russia, Canada haihitaji kulitambulisha Jeshi lake.
3. Switzerland
Switzerland ama Uswisi ina wanajeshi 150,000 na ndege za kivita 156. Wanajeshi hawa hutakiwa kuishi na silaha zao za kijeshi majumbani kwao. Nchi hii pia imezungukwa na Mataifa yenye nguvu Ujerumani, Italia, Ufaransa na Austria ambazo ni washirika wake wakati wa vita.
2. Japani
Japan ina wanajeshi 250,000 na zaidi ya vifaru 600. Ni nchi yenye cha anga kinachotambulika kama kikosi kikubwa cha tano cha anga duniani na chenye teknolojia kubwa kikiwa na ndege 1,590. Mwaka 2016 Serikali ya Japan ilitumia takriban Dollar Bilioni 600 za Marekani kwa ajili kuimarisha Jeshi lake.
1.Marekani
Serikali ya Marekani hutenga Dollar Bilioni 596 kwa ajili ya Jeshi lake ikiwa ni Bajeti za nchi Saba na ni 80% ya Bajeti nzima ya Serikali ya Urusi. Marekani inasemekana kuwa na silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuuwa kila mtu duniani.