Wakazi wa Kimara Dar es Salaam wamelalamika juu ya bomoa bomoa inayoendelea kufanywa na Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads kubomoa nyumba zilizopo kwenye hifadhi ya barabara huku wakidai muda ambao walipewa haukutosha.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo Omary Abdallah Ngwena amesema TANROADS walifika eneo hilo April mwaka huu na kuweka alama za X katika nyumba zao na jana mchana Mahakama Kuu ilitoa agizo la kuzuiwa kwa zoezi hilo kusikiliza kesi ambayo ilifunguliwa tangu mwaka 2012 lakini leo nyumba zao zimebomolewa.
>>>”Hata tulipomwambia Msimamizi Mkuu wa zoezi hili leo kuhusiana na agizo la Mahakama alisema hajapewa taarifa zozote za kusimamishwa kwa zoezi hilo na hivyo kuendelea kubomoa. Vitu vyetu nimeharibiwa sana kwa sababu hatukujipanga kuhamisha vitu kutokana na agizo la Mahakama.” – Omary Abdallah Ngwena.
Uliikosa hii?WEMA SEPETU TENA: Ni kuhusu kesi yake Mahakamani