Baada ya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi lililokuwa limewekwa na baraza la wadhamini wa club ya Simba la kutaka mkutano Mkuu wa Simb SC uliyofanyika August 13 usifanyike lakini baada ya mkutano kufanyika walimsimamisha mzee Hamisi Kilomoni uanachama na kumuondoa katika baraza la wadhamini.
Mzee Hamisi Kilomoni alikuwa ni mmoja wa viongozi wa bodi ya wadhamini waliyokuwa wanapinga mpango wa Simba SC kubadili mfumo wa kiuendeshaji kutoka wa sasa na kuingia katika hisa, kwa madai ya kuwa club atapewa mtu mmoja.
Baada ya kusimamishwa uanachama na kuondolewa katika baraza la wadhamini mzee Kilomoni ameongea na waandishi wa habari leo “Mimi ndio mdhamini wa club ya Simba ndio mdhamini asilia sio wa kuokotwa tu kutoka kusikojulikana” >>> Kilomoni
“Mimi ni mdhamini ambaye nimeichezea club yangu, nimeilea, nimeitumikia club yangu, mimi ni kila kitu na sasa hivi ndio mdhamini wa club ya Simba na mimi ni mdhamini sio tu kwa kuniokota kutoka barabarani hapana, walinipa kutokana na matendo yangu” >>>> Kilomoni
“Leo nisingependa kuongea sana kuhusiana na hiki kinachoendelea kutokana kuna kitu kimoja sijakipata mkononi kwangu, najua waandishi mmesikia sana mzee Kilomoni kafutwa lakini sijapata barua sio sahihi, hii sio mara ya kwanza kusema wamenitoa hadi nipate barua” >>> Kilomoni
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0