Baada ya headlines za Simba kufanyiwa mabadiliko na kutolewa semina kwa wanachama wote juu ya mfumo huo, wanachama wa club ya Simba SC leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Posta Dar es Salaam, wamefanya mkutano mkuu wa kuridhia mabailiko ya mfumo.
Katika mkutano mkuu wa Simba uliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuhusiana na kubadili mfumo wa uendeshaji wa club wa sasa na kwenda katika mfumo wa hisa unaotumiwa na vilabu vya Man United, Arsenal na vingine baranu Ulaya umeafikiwa na wanachama.
Jumla ya wanachama 1216 wa club ya Simba waliyokutana leo katika mkutano mkuu wa meafiki mfumo wa hisa na kuunga mkono kwa asilimia 100, huku mwanachama mmoja ndio hajaunga mkono.
Simba wakiingia katika mfumo huo asilimia 50 za hisa wako radhi zimilikiwe na mtu mmoja, asilimia 9 watagawana wanachama hai, asilimia moja wazee wa Simba waliyoitoa mbali club hiyo na asilimia 40 nyingine zitauzwa ila kwa sharti la aliyenunua asilimia 50 za mwanzo haruhusiwi, yeye au jamaa yake kununua hisa nyingine.
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0