Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kupitia fedha za marejesho ya pikipiki za UBOJA ‘Revolving Funds’ amesema wanawake 500 wa Arusha wanaotegemea kuanza biashara ndogondogo watawezeshwa kwa ajili ya kujikimu kimaisha kwa kuwapa mkopo wa Tsh. 200,000 kwa masharti nafuu na hautokuwa na riba.
RC Gambo amesema lengo kuu la mkopo huo ni kwa mwanamke mmoja mmoja au kundi la wanawake watakaotimiza vigezo ambapo wataanza na wanawake 500 kutokana na marejesho ya Milioni 100 baada ya vijana wa bodaboda kurejesha.
>>>“Tumesema tuanze na akina mama 500. Kwa hivyo, na wenyewe pia tukasema tutawapatia Milioni 100. Nilifikiria kuwasaidia akina mama kwanza, mama yangu amenisomesha kwa kuuza uji. Nimezaliwa na kukulia Kariakoo.” – RC Gambo.
VIDEO: Tamko la kituo cha sheria kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu