Nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea Azam FC Himid Mao mwezi May 2017 alienda kufanya majaribio katika club ya Randers FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark, Himid Mao alifanya majaribio na ikaripotiwa kuwa amefuzu majaribio yake ndani ya Randers FC.
AyoTV leo imefanikiwa kumpata katika exclusive interview Himid Mao na kumuuliza vipi mpango wake wa kujiunga na Randers FC umekaaje, maana dirisha la usajili barani Ulaya linakaribia kufungwa mwisho wa mwezi huu?
“Ile timu ilikuwa ikinifuatilia kwa muda mrefu zaidi ya mwaka nilikuwa niende kusaini moja kwa moja msimu wa mwaka juzi, kwa sababu walikuwa wanatafuta mtu wa nafasi yangu na mwenye sifa kama zangu lakini nikashindwa kwenda kutokana na Azam tulikuwa tupo katika ratiba ngumu” >>> Himid Mao
“Mwalimu (Stewart Hall wa Azam FC) akasema huyu nitamtumia, japo mechi ya hapa ya confederation sikucheza na mechi ya kule nilicheza dakika chache, baadae nilivyoongea na mwalimu akaniambia focus yangu haipo katika mpira ndio maana hakunipanga” >>> Himid Mao
“Safari hii wakaniita baada ya kuwasiliana na wakala wangu maana walikuwa wanajiandaa kwa Europa, nikaenda kucheza nao mazoezi na mechi za kirafiki wakatuma ripoti kwa wakala wangu kuwa nimefuzu lakini si unajua suala la bajeti kwa hiyo wanahitaji aondoke mtu ili niingie kwa hiyo nasubiri” >>> Himid Mao
EXCLUSIVE: Himid Mao amezungumzia John Bocco kuondoka Azam FC