Japokuwa sekta ya elimu bado inakabiliwa na changamoto nyingi barani Afrika, vipo vyuo ambavyo vimekuwepo katika bara hili kwa miaka mingi na ni jambo la kujivunia sana. Vifuatavyo ni Vyuo Vikuu vikwonge zaidi barani Afrika.
10. Chuo Kikuu cha Ghana
Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1948 ambacho kwa kipindi hicho kiliitwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Gold Coast ambayo kwa sasa ni Guinea kabla ya kufanywa Chuo Kikuu mwaka 1961 na hadi sasa kinasajili wanafunzi 40, 000 kila mwaka.
9. Chuo Kikuu cha Ibadan
Chuo hiki kilichopo nchini Nigeria kilianzishwa mwaka 1948. Ni chuo cha kwanza kuwa katika orodha ya vyuo bora 1000 vya elimu ya juu na kuingia kwenye orodha ya vyuo vikuu 100 bora duniani.
8. Chuo Kikuu cha Makerere
Ni chuo kikubwa na kikongwe kuliko vyote nchini Uganda. Kilianzishwa mwaka 1922 kama shule ya ufundi iliyotoa kozi za useremala, ujenzi na ufundi gereji na baadaye kukua kwa kasi na kuanza kufundisha masomo ya udaktari, ualimu, kilimo na mengineyo.
7. Chuo Kikuu cha Algiers
Chuo hiki kiko nchini Algeria na kilianzishwa mnamo mwaka 1909. Kinafahamika kama chuo mama cha nchini humo na kilianzishwa kama kwa mfumo wa shule nne na hadi leo kinafundisha wanafunzi zaidi ya 10,000. Kwasasa ina vitivo sita ambavyo ni vya Sheria, Udaktari, Sayansi ya Jamii, Masomo ya Dini, Herufi na Lugha pamoja na Usimamizi na Sayansi ya Uchumi.
6. Chuo Kikuu cha Cairo
Ni chuo ambacho kipo nchini Misri na kilianzishwa mwaka 1908 hapo nyuma kikijulikana Chuo Kikuu cha Misri na baadaye Chuo Kikuu cha Faud. Kwa sasa chuo hiki kina wanafunzi 280,000 na vitivo 18 na kinasemeka kuwa moja ya vyuo vikuu vinavyo sajili wanafunzi wengi sana kila mwaka duniani kote.
5. Chuo Kikuu cha StellenBosch
Chuo hiki kilianzishwa nchini Afrika Kusini mwaka 1866. Ni chuo kikuu cha utafiti na kinajulikana kuwa chuo kikongwe kuliko vyote sawa sawa na Chuo Kikuu cha Cape Town katika nchi za chini ya Jangwa la Sahara. Kina wanafunzi 30, 000.
4.Chuo Kikuu cha Cape Town
Kinapatikana nchini Afrika Kusini na kilianzishwa mwaka 1829 kama Chuo Kikuu Kishiriki za Afrika Kusini. Chuo hiki kilianza kama shule ya sekondari ya wavulana na baada ya kupokea michango mbalimbali ndipo chuo kikuu kilipoanzishwa. Kwa sasa kina sajili wanafunzi 27, 000 ila mwaka.
3. Chuo Kikuu cha Sierra Leone
Chuo hiki kipo nchini Sierra Leone na kilianzishwa na jamii ya wamishenari kama shule ya wamishenari wa kanisa la Anglikana mwaka 1876. Chuo hiki kinatajwa kuwa chuo kikongwe kuliko vyote kwa nchi za Magharibi mwa Afrika.
2. Chuo Kikuu cha Al-Azhar
Hiki kilianzishwa kama chuo cha elimu ya kiislamu yaani Madrasa mnamo mwaka 970-972 AD yaani wakati wa Yesu. Ni chuo cha Kiislamu kilichopo Misri na kwa sasa kina wanafunzi karibu 90,000. Maktaba yake ni ya pili kwa umaarufu na cha pili kama chuo kikongwe kinachotoa shahada baada ya Chuo Kikuu cha Cairo.
1. Chuo Kikuu cha Al-Karaouine
Chuo hiki kipo nchini Morocco. Kilianzishwa mnamo mwaka 859 AD na ni chuo ca kwanza zha Kiislamu. Kimewekwa kwenye Kitabu cha Dunia cha Kumbukumbu na Shirika la Kimataifa la Unesco limekitambua kama Chuo Kikuu kikongwe duniani na ambacho kinaendelea kutoa elimu.
Uliiona hii? JE STEVE NYERERE ALISHAYAMALIZA NA MAMA WEMA?