Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka wadau na watafiti mbalimbali kufanya tafiti zao na kuzihusianisha na maisha halisi ya jamii kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo ili kuchochea maendeleo kwa kuwa tafiti nyingi haziunganiki na mazingira halisi.
Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, RC Mongella amefungua mkutano wa Wanachama 60 wa Umoja wa Watafiti wa Taasisi za Kitaifa, Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyosaidia kukuza na kuimarisha Utafiti na Ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi waliokutana Mwanza kujadili changamoto mbalimbali za Kitafiti zinazofanywa Kanda ya Afrika.
ULIPITWA? Serikali imekichukua kiwanda cha Ngozi Africa Tanneries, Mwanza…tazama kwenye hii video!