Katika kuhakikisha kuwa wateja wake na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, naambiwa kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza good news kwa wateja wake kwa kupunguza bei za vifurushi vyake vyote na kuboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hasa vya bei ya chini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, amewabainishia wateja wa DStv katika Makao Makuu ya kampuni hiyo Dar es Salaam akisema good news hiyo itaanza kutumika rasmi September 1, 2017.
>>>”Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei. Tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao. Leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote.”
Akifafanua zaidi kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema kumekuwa na punguzo la hadi 16% ikiwa ni punguzo kubwa sana litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv na kuzitaja bei mpya ambazo ni;
Bei Mpya za vifurushi vya DStv
Kifurushi | Beiyasasa | BeiMpya | % YaPunguzo |
Premium | TZS 184 000.00 | TZS 169 000.00 | 8.15% |
Compact Plus | TZS 122 500.00 | TZS 109 000.00 | 11.02% |
Compact | TZS 82 250.00 | TZS 69 000.00 | 16.11% |
Family | TZS 42 900.00 | TZS 39 000.00 | 9.09% |
Access (Bomba) | TZS 19.975.00 | TZS 19 000.00 | 4.88% |
ULIPITWA? Polisi aliyetoweka siku mbili akutwa amefariki Ziwa Victoria