Leo August 31, 2017 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imezindua mfumo mpya wa kufanya malipo ya huduma kwa njia ya kielektroniki ambao utatupilia mbali malipo ya pesa taslim na malipo kuanza kufanywa kwa kutumia kadi maalumu au simu za mkononi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili Prof. Lawrence Maseru mfumo huu unalenga kusimamia ukusanyaji mzuri wa mapato yanayotokana na malipo ya huduma hizo ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.
“Mfumo huu pia utasaidia kupunguza adha kwa wagonjwa ya kufanya malipo kwa kukaa muda mrefu kwenye foleni ukizingatia hospitali hii inatoa huduma kwa watu zaidi ya elfu mbili kwa siku, hivyo mfumo huu mpya utapunguza adha wanazokabiliana nazo wagonjwa kila siku.”
Ulipitwa na hii? TWAWEZA!! Ya kufahamu ripoti mpya hali ya Afya Tanzania
VIDEO: Ya kufahamu kwenye taarifa ya Haki za Binadamu na Biashara mwaka 2016