Viongozi na wananchi katika vijiji vya Ololosokowani na Kiritalu vilivyopo Ngorongoro wamemuomba Rais Magufuli kuingilia kati kusitisha zoezi la Askari wa Wanyamapori kukamata ng’ombe 1,000 na kuchoma moto nyumba zaidi ya 500 kwa madai ya kuvamia eneo la Hifadhi
Diwani wa Kata ya Ololosokowan, Yannick Ndoinyo alisema>>>”Karibu wamekosa imani na sisi kama viongozi, hawataki tena kutusikiliza tena kabisa kwa sababu tunakosa majibu ya matatizo yao. Huko tunakokwenda kutafuta majibu hatupati, lakini mimi ninachoomba Serikali kwanza isimamishe operesheni inayoendelea. Tunamuomba Rais asaidie kuchukua hatua.” – Ndoinyo.
Aidha, Ayo TV na millardayo.com zimempata Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye amekiri kukamatwa mifugo na kusema watu wataendelea kuondolewa katika eneo hilo kwa kufuata sheria.
>>>”Hii yote ni propaganda inayofanywa na hizi NGOs maana kazi yake ni kuhakikisha kuna mgogoro hapo Loliondo. Wakiutangaza huo mgogoro wanaendelea kupata fedha kwa wafadhili wao. Tunachosema ng’ombe hawatarudi tena ndani na kwa sababu hiyo mgogoro huo hautakuwepo tena.
“Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita ng’ombe kama 940 hivi waliingizwa kwa kuchochewa na hizo NGOs, na walivyoingizwa walikamatwa na wako Mahakamani.” – Prof. Maghembe.
SHAMBULIZI: Diwani arushiwa mishale Karagwe