Moja ya stori ambazo zilikamata headlines siku za hivi karibuni ilikuwa ni kuhusu ya Wabunge nane wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi, CUF kufutwa uanachama kisha chama hicho kuteua Wabunge wangine kuziba nafasi zao.
Sasa taarifa iliyonifikia ni kuwa mmoja kati ya Wabunge nane wateule, Bi. Hindu Hamis Mwenda amefariki jana jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kisukari.
Bi. Hindu alikuwa mmoja wa Wabunge nane wa Viti Maalum waliotakiwa kuapishwa na Bunge September 5, 2017 baada ya kuteuliwa na CUF na kuthibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi July 27, 2017 kuchukua nafasi ya Wabunge nane wa Viti Maalum waliofutwa Uanachama wa chama hicho licha ya uteuzi wao kupingwa Mahakamani.
Mbunge mteule Viti Maalum CUF, Hindu Hamis Mwenda amefariki jana. Aliteuliwa kuziba nafasi moja ya Wabunge waliofutwa CUF #MillardAyoUPDATES
— AyoTV (@ayotv_) September 2, 2017
ULIPITWA? Maamuzi ya Mahakama Kuu ile kesi ya Wabunge 8 waliofutwa CUF…tazama hapa kenye hii video!!!
ULIPITWA? MAHAKAMA KUU KUHUSU WALE WABUNGE 8 WA CUF!!!